Mabadiliko sera ya Wazee ipo mbioni

Na Sarah Moses, Dodoma.

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi maalum ipo katika hatua za Mwisho za kukamilisha mabadiliko ya sera ya wazee ambapo miongoni mwa maboresho yatakayozingatiwa ni pamoja na umuhimu wa jamii kujiandaa kabla ya uzee.

Hayo ameyasema leo Bungeni Mei 17 ,2024  Waziri wa wizara hiyo Dkt.Dorothy Gwajima wakati alipokuwa akiwasilisha Bungeni bajeti ya makadilio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2924/2025

Maboresho mengine ni huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa wazee, miundombinu na mazingira wezeshi kwa wazee na uwezeshwaji wa wazee kwenye mabadiliko ya Teknolojia kama TEHAMA. 

Amesema hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya wazee 574,321 (Me 214,739, Ke 359,582) ambapo kati yao wazee wasiojiweza 365,284 (Me 145,829, Ke 219,455) sawa na asilimia 63.6 ya wazee wote waliofanyiwa tathmini, wamepatiwa vitambulisho maalum kwa ajili ya msamaha wa matibabu. 

Vilevile, kampeni ya “MPISHE MZEE KWANZA” inaendelea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Taifa ili kutoa kipaumbele na kuhakikisha wazee wanapata huduma za afya kwa wakati. 

“Kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024 kulikua 

jumla ya madirisha 1,066 ya huduma kwa wazee 

nchini kote ikilinganishwa na madirisha 629 

yaliokuwepo mwaka 2022/2023 ikiwa na ongezeko la 

madirisha 437 sawa na asilimia 69.48.”amesema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *