Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA), imetoa angalizo ya mvua kubwa kunyesha katika mikoa 12 ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Taarifa iliyotolewa jana na TMA, ilisema mvua hizo zitanyesha kwa siku mbili kuanzia leo zitahusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dar es Salaam, Tanga, Pwani (Visiwa vya Mafia), Songwe, Njombe Ruvuma, Morogoro, Lindi, Mtwara Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, athari zinazoweza kujitokeza ni makazi ya watu kuzungukwa na maji, kuathirika kwa baadhi za maeneo ya kiuchumi.
Hata hivyo, kesho mvua hizo zinatarajia kunyesha katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dar es Salaam, Tanga, Pwani (Visiwa vya Mafia), Songwe, Njombe Ruvuma, Morogoro, Lindi, Mtwara, Unguja, Pemba.
TMA imewataka wananchi kuzingatia utabiri huo na kujiandaa kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.