Simba SC yatambulisha ‘jembe’ jipya kutoka JKU

Na Badrudin Yahaya

KLABU ya Simba, imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa JKU, Saleh Karabaka kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mchezaji huyo ni usajili wa kwanza kwa Simba kwenye dirisha hili dogo la usajili chini ya Kocha wao, Abdelhak Benchikha.

Karabaka anajiunga na Simba ikiwa zimebaki saa chache kabla ya timu hiyo kucheza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya Mapinduzi dhidi ya JKU.

Kwa klabu ya JKU ambayo inashiriki Ligi ya Zanzibar, anakuwa mchezaji wa pili kuondoka klabuni hapo katika dirisha hili la usajili.

Awali wapinzani wa Simba, Klabu ya Yanga walifanikiwa kunasa saini ya kiungo, Shekhan Ibrahim akitokea timu hiyo.

Simba bado wapo katika maboresho ya kikosi chao kwenye dirisha hili na wanatarajia pia kuongeza wachezaji wengine zaidi kwa mujibu wa taarifa kutoka katika uongozi wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *