Ajali ya basi, treni yaua 13

*Imehusisha Basi la Ally’s, majeruhi 32

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WATU sita wamefariki dunia, wengine 32 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Basi la Kampuni ya Ally’s Star kugonga kichwa cha treni ya mizigo na kupinduka.

Ajali hiyo imetokea jana, basi hilo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kwenda mkoani Mwanza na kugonga treni hiyo katika makutano ya barabara ya reli Manyoni-Singida.

Taarifa zinasema, chanzo cha ajali hiyo n mwendo kasi wa dereva wa basi

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dkt. Furaha Mwakafilwa, alisema walipokea miili ya watu 13 pamoja na majeruhi 32.

Hata hivyo, kamanda wa Polisi mkoani Singida, Stella Mutabihirwa, alisema majeruhi ni 34 wakati Shirika la Reli Tanzania (TRC) likisema majeruhi ni 25.

Mkuu wa Mkoa huo, Peter Serukamba, alisema hakuna majeruhi aliyesalia ndani ya basi baada ya kuinuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya TRC, lilisema basi hilo lenye namba T 178 DVB liligonga kichwa cha treni chenye namba V951 9006 na kuacha njia ya reli.

Treni hiyo ilikuwa ikitokea Stesheni ya Aghondi kwenda Manyoni ambapo waliofariki ni wanawake sita, wanaume saba na kuwasihi madereva kufuata sheria na alama za usalama katika njia za reli ili kuepusha ajali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *