Mwinyi afafanua maana ya uwekezaji

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema uwekezaji ni hali ya watu kuleta miradi katika nchi husika.

Amewatoa hofu wananchi kuhusu uwekezaji akisema wanufaika ni wananchi wenyewe, kupata fursa ya ajira.

Rais Dkt. Mwinyi aliyasema hayo jana katika Jukwaa la Fikra la kuangazia miaka mitatu ya uongozi wake katika upande wa mafanikio, fursa na changamoto.

Alisema ndani ya miaka mitatu wamejitahidi kutekeleza yote waliyodhamiria kuwatumikia wananchi wa Zanzibar.

Aliwataka wananchi wa Zanzibar wasiogope kuwekeza, watapatiwa unafuu katika uwekezaji huo.

Aliongeza kuwa, katika kuwatumikia wananchi mitihani ni sehemu ya maisha lakini lengo kuu ni kuleta amani ndio maana sababu ya kuanzisha serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo.

Alieleza kuwa, changamoto iliyopo ni utendaji wa baadhi ya viongozi ambao hawataki mabadiliko lakini hakukata tama, ameendelea kupiga hatua.

“Katika uongozi lazima uwe na utawala bora ambao unafuata Katiba na sheria, kushirikisha watu kufanya maamuzi yenye tija ndani yake,” alieleza.

Alisema wananchi wamechagua viongozi ambao watafanya maamuzi ambayo yataonyesha njia hivyo dhamira njema aliyonayo kwa kwa wananchi ni kuleta matokeo sahihi kwao.

Alisisitiza kuwa, uongozi bora lazima utoe fursa ya kusikiliza na kushirikisha wananchi katika kuleta mabadiliko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *