Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 3 zenye mazingira mazuri ya uwekezaji barani Afrika.
Kwa mujibu wa utafiti mpya uliotolewa na wawekezaji wa kimataifa na wa ndani umeeleza Tanzania ni nchi ya tatu bora zaidi iliyopendelewa zaidi kwa uwekezaji na Afrika Mashariki.
Utafiti huo umefafanua kuwa Tanzania inaongozwa na nchi mbili ambazo ni Afrika Kusini na Nigeria ambapo namba nne inashikiliwa na Ghana, Kenya, Mauritius, Zambia, Uganda, Msumbiji pamoja na Zimbabwe.
Asilimia 80 ya wawekezaji walisema wanapendelea kufanya uwekezaji nchini Nigeria asilimia 30 na Afrika Kusini asilimia 50 katika siku zijazo, kwa nchi mbili zenye idadi uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.
Aidha, wawekezaji hao walipendelea kuwekeza Tanzania asilimia 15, Ghanaa silimia 14 na Kenya asilimia 14 zikiingia kwenye orodha ya 5 bora ya maeneo yanayopendelewa kwa uwekezaji.
Miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa zaidi kwenue uwekezaji ni mafuta na gesi, bidhaa, madini, viwanda na biashara, teknolojia, dawa, huduma za kifedha, mawasiliano, bima, kilimo, ujenzi, uzalishaji umeme, makazi, habari usafirishaji.
Falsafa ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kukuza uwekezaji na kujenga maridhiano kupitia 4R (Ustahimilivu, Mageuzi , Maridhiano na Ujenzi mpya) ndiyo kitambulisho kinachomtambulisha Rais Samia kuwa gwiji wa siasa za maridhiano.
Katika hilo, Rais Samia aliwataka Watanzania kulinda misingi ya demokrasia na uhuru wa watu pamoja na vyombo vya habari.
Katiak siku 100 za kwanza akiwa madarakani, Rais Samia alionesha uimara wake katika kurejesha masuala ya uhusiano wa kimataifa kwa wanadiplomasia.
Akiwa madarakani Rais Samia alifanya mikutano na viongozi wote wa taasisi za kimataifa kwenye maeneo ya uchumi, uhusiano wa kimataifa na fedha.
Lakini pia amefanya ziara nyingi kwenye mataifa kadhaa ulimwenguni kati ya amsuala anayofanya rais Samia katika ziara hizo ni kukutana na mamlaka za jumuiya ya wawekezaji na wafanyabaishara wa anakotembelea.
Katika mambo ya msingi kwenye diplomasia ya uchumi ni kuvutia uwekezaji kutoka nchi nyingine kwa kujua fursa za uwekezaji zilizopo katika nchi, miradi inayotekelezwa kuanzia ngazi ya Kata hadi kitaifa jambo ambalo Rais Samia hulifanya anapokua kwenye ziaar zake.
Licha ya ziara za nje, akiwa kwenye ziara za ndani Rais Samia amekuwa akizindua na kukagua miradi ya maendeleo ambayo imekuwa ikifanywa hapa nchini katika sekta za madini, viwanda, biashara, kilimo, elimu, maji, nishati, madini, uwekezaji, ambayo imekuwa na matokeo chanya kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.