Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Roda Peter (30) mkulima na mkazi wa Kihonda kwa kosa la kuangamiza vichanga viwili vyenye jinsia ya kike na kiume vinavyokadiriwa kuwa na umri wa siku moja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Oktoba 12, 2023 maeneo ya Kihonda ambapo mtuhumiwa aliviweka vichanga hivyo kwenye mifuko miwili ya salfeti mweupe na mweusi kisha kuvitupa kwenye kichaka ambapo vilikutwa vikiwa vimefariki.
“Kuna mama alijifungua na kutupa na kutupa Watoto wake wachanga ambao ni mapacha, katika upelelezo wetu kwa kushirikiana na wananchi tulifanya ufuatiliaji na kumbaini huyo mama tumefanikiwa kumkamata,” alisema.
Katika hatua nyingine, Oktoba 16 jeshi hilo lilimkamata Glory Barnabas (23), mkulima na mkazi wa Tungi kwa kosa la wizi wa mtoto wa kike anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi mitatu aliemuiba Septemba 2023 kutoka kwa mama mwenye matatizo ya afya ya akili,”alisema.
Kamanda Mkama alisema jeshi hilo linamshikilia Emmanuel Charles (22) ‘Malupelupe’, mkazi wa mafisa na wenzake 5 kwa kosa la wizi wa kukwapua (vichandu).
Alisema Oktoba 13, 2023 majira ya saa 4 usiku huko maeneo ya Miswala katika manispaa na mkoa Maragama watuhumiwa wakitumia pikipiki aina ya Haojue yenye namba za usajili MC 270 DMS walipora simu ndogo aina ya Tecno yenye thamani ya sh 30,000 na pesa sh 50,000.
Alisema watuhumiwa hao walipo pekuliwa walikutwa na pikipiki mbili aina ya Haojue zenye namba za usajili MC 270 DMS na MC 414 CTW wanazotumia kufanya uhalifu.
Watahimiwa hao walikutwa na simu moja ndogo ainu ya tecno, makasha ya simu 13, pochi za kike 16 na simu janja 10 za aina mali ambazo zimeibiwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
Aidha, alisema katika kusimamia sheria za usalama barabarani jumla ya madereva 10 wa magari yanayo safirishwa nje ya nchi maarufu kama (IT) na ambayo hayajasajiliwa wamekamatwa wakiwa wamebeba abiria kinyume cha shera na madereva wote wamefikishwa mahakamani kwa hatua za kesheria.
Alisema jeshi hilo limekamatwa gari aina ya Fao yenye namba za usajili T627 DZH tela namba T 130 AAY mali ya Ahmed Said Islam (58) mfanyabiashara na mkazi wa Uhindini ikiendeshwa na Raheem Ramadhani (45) mkazi wa Mlimani boma wilaya ya Kilosa likiwa na vyuma mbalimbali mali idhaniwayo kuwa ya umma ambavyo ni vipande vya nondo 263 na mataruma ya reli 37 ikiwa inasafirisha vyuma hivyo ikitokea Wilaya Kilosa mkoa Morogoro kuelekea Dar-es-Salaam.