Serikali yahadharisha kutokea kwa Tsunami

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam

OFISI ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura imetoa tahadhari ya Tsunami inayoweza kusababishwa na mlipuko wa Volcano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana ilieleza kuwa Tsunami hiyo inaweza kutokea katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kikiwa na kiwango kikubwa cha kutokea.

Aidha, taarifa hiyo ilifafanua kuwa kuna uwezekano wa kutokea madhara kwa kutokea mawimbi ya Tsunami na kuweza kuathiri.

Hata hivyo taarifa hiyo iliesema hatua zinapaswa kuchukuliwa kwa watumiaji wa bahari na waakzi wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki.

Pia mamlaka husika zinashauriwa kujiandaa na kuchukua tahadhari ni za Mkoa wa Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara na Dar es Salaam, Jeshi la Polisi Maji, Jeshi la Zimamoto, TRCS, DarMAERT, Manispaa na halmashauri zote.

Katika hatua nyingine, Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA), imetoa angalizo la mvua kubwa inayoweza kutokea katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma kwa siku 3.

Angalizo hilo limetolewa kuanzia Oktoba 19, 2023 hadi Oktoba 21, 2023.

Mamlaka hiyo imeeleza uwezekano wa kutokea kwa mvua hiyo na athari zinazoweza kutokea ni wastani.

Ilieleza kuwa, athari ambazo zinaweza kutokea ni baadhi ya makazi kujaa maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi hivyo wananchi wajiandae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *