Na Salha Mohamed, Singida
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo anaanza ziara ya siku mbili mkoani Tabora akitokea mkoani Singida.
Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Samia atatembelea Wilaya za Igunga na Nzega mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Batilda Buriani, baada ya mapokezi, Rais Dkt. Samia ataweka jiwe la msingi katika Chuo cha VETA kilichogharimu sh. bilioni 2.612.
Baada ya tukio hilo, Rais Dkt. Samia atazungumza na wananchi katika uwanja wa Barafu.
“Akimaliza mkutano, Rais atatembelea shamba la mbegu Kilimi katika Wilaya ya Nzega kuangalia teknolojia ya umwagiliaji iliyofungwa katika shamba hilo,” alisema.
Shamba hilo lina ukubwa wa ekari 1,000, limewekwa mitambo ya umwangiliaji kwa gharama ya sh. bilioni 6.2.
Kufungwa kwa mitambo hiyo kutasaidia shamba hilo kuzalisha mbegu muda wote wa mwaka, kuongeza tija. Hata hivyo, Dkt. Buriani aliwataka wananchi mkoani humio kujitokeza kwa wingi katika ziara hizo.