Ni fainali ya kisasi Djokovic, Alcaraz Cincinnati Open

CINCINNATI, Marekani

MCHEZAJI nyota katika tenisi, Novak Djokovic, amepata nafasi ya kulipa kisasi cha kufungwa katika fainali ya Wimbledon na Carlos Alcaraz wakati wawili hao watakapoumana katika fainali ya Cincinnati Open.

Nyota huyo namba moja duniani, Alcaraz, alitinga fainali juzi baada ya kumchapa Mpoland, Hubert Hurkacz kwa seti 2-6 7-6 (7-4) 6-3 katika nusu fainali.

Kisha nyota namba mbili duniani, Djokovic alimtandika Mjerumani, Alexander Zverev kwa seti 7-6 (7-5) 7-5 na kumfuata Alcaraz fainali.

“Ni changamoto kubwa kwangu kwa sasa,” amesema Djokovic.

Mhispania, Alcaraz, 20, alimchapa mserbia huyo katika seti tano mwezi uliopita na kutwaa taji la Wimbledon na ameshinda mechi mbili kati ya tatu walizokutana.

“Ni kipimo kizuri kuelekea michuano ya US Open,” alisema Djokovic, 36,. “Ni wazi hali ipo tofauti.

“Kwasasa utakuwa ni mchezo wa kwanza kuchezwa katika udongo kati yetu.

Ushindi wa Alcaraz dhidi ya Hurkacz, ina maana amecheza fainali nane kwa mwaka huu. Pia amekuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza fainali ya Cincinnati Open tangu alivyofanya Pete Sampras mwaka 1991 akiwa na miaka 19.

Pia Djokovic, 36, atakuwa mchezaji mkubwa zaidi kutwaa taji la Cincinnati katika karne hii mbali na Ken Rosewall, 35, aliyetwaa ubingwa mwaka 1970.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *