Mbappe kutofanya mazoezi na PSG

PARIS, Ufaransa

STRAIKA Kylian Mbappe, hatofanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Paris St-Germain wakati wakianza mazoezi jana kuelekea msimu mpya wa Ligue 1.

Mbappe amekuwa katika mzozo mkubwa na PSG kuelekea kutimiza ndoto zake za kujiunga na Real Madrid.

Mfungaji Bora huyo wa muda wote ndani ya klabu hiyo, amekataa kuongeza mkataba huku ule wa awali ukimalizika msimu ujao.

Kutokana na hilo, PSG imepanga kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa sasa kuliko kumuachia aondoke huru atakapomaliza mkataba wake.

Kutokana na hilo, Mbappe aliachwa na PSG katika maandalizi ya msimu mpya katika ziara yao barani Asia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *