Svitolina, Azarenka wazuiwa kusalimiana DC Open

WASHINGTON, Marekani

WATAZAMAJI wa michuano ya DC Open, wamewaonya mchezaji wa Ukraine, Elina Svitolina kutoshikana mikono na Victoria Azarenka wa Belarus.

Wakati wa mgogoro wa Urusi na Ukraine, Svitolina, alikataa kusalimiana na wapinzani wake wanaotoka Urusi au Belarus.

Azarenka alizomewa baada ya Svitolina kumchapa wakati wa michuano ya Wimbledon na alinusurika kurudia hivyo, mwisho wa mchezo huo ubao ulisoma Svitolina alishinda kwa seti 7-6 (7-2) 6-4 katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo jijini hapa.

“Ni vitu sahihi,” anasema Svitolina ambaye kwa ubora wa viwango vya Dunia ni wa 27.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *