Fabinho amfuata Benzema Al-Ittihad

JEDDAH, Saudi Arabia

KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Fabinho, amekamilisha uhamisho wa kujiunga na AL-Ittihad ya Saudi Arabian akitokea Liverpool kwa mkataba wa miaka mitatu.

Nyota huyo, 29, hakusafiri na timu hiyo katika kambi ya hivi karibuni Ujerumani baada ya miamba hiyo kulipa pauni milioni 40.

Pia Fabinho aliachwa katika ziara ya hivi karibuni ya timu hiyo nchini Singapore wakati akiendelea kukamilisha baadhi ya vitu katika uhamisho huo.

Akiichezea mechi 29 kwa taifa lake, alijiunga na Liverpool Julai, 2018 akitokea Monaco kwa ada iliyokaribia pauni milioni 39.

Fabinho anasema anaondoka nyumbani kwao baada ya kuichezea timu hiyo kwa heshima kubwa na furaha kwa miaka mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *