Pambano la Smith, Beterbiev lafutwa

QUEBEC, Canada

PAMBANO la ubingwa la bondia Muingereza, Callum Smith dhidi ya bingwa wa WBC, WBO na IBF uzito wa juu mwepesi, Artur Beterbiev mjini Quebec Agosti 19, limefutwa.

Beterbiev, 38, ambaye hajawahi kupigwa, amefanyiwa upasuaji wa taya.

Smith, 33, alijitosa katika uzito huo baada ya kupoteza pambano lake la uzito wa kazi mkanda wa WBA dhidi ya Saul ‘Canelo’ Alvarez Desemba, 2020.

Amepangiwa kuzichapa na Beterbiev baada ya kushinda pambano lake la mtoano dhidi ya Mathieu Bauderlique Agosti, mwaka jana.

Beterbiev ambaye ni mzaliwa wa Urusi na kukulia Canada, hajapigwa katika mapambano 19 na ndiye bingwa wa Dunia mwenye wastani wa asilimia 100 kushinda kwa KO.

Smith alipoteza kwa Alvarez ikiwa ndio pambano pekee alilopoteza katika maisha yake ya mchezo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *