Nkunku wa moto, Disasi atua

MARYLAND, Marekani

TIMU ya Chelsea, imetwaa ubingwa wa michuano maalum kujiandaa na msimu mpya baada ya kuitandika Fulham 2-0 uwanjani FedEx Field mjini hapa.

Beki mkongwe, Thiago Silva, alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 20 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Ben Chilwell.

Straika mpya, Christopher Nkunku, alifunga bao la pili kabla ya mapumziko kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Carney Chukwuemeka.

Hilo ni bao lake la tatu kwa Nkunku katika mechi hizo za kujiandaa na msimu baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 52 akitokea RB Leipzig.

Mchezo huo ulipigwa kwenye uwanja wa timu ya Washington Commanders inayocheza timu ya NFL.

Katika hatua nyingine, Chelsea, imekubali kutoa ada ya pauni milioni 38.6 kwa ajili ya kumsajili beki wa AS Monaco, Axel Disasi.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Disasi, 25, atakuwa ameongeza wigo wa mabeki wa kulia ndani ya timu hiyo baada ya kuumia kwa Wesley Fofana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *