Muundo Mwenge wa Olimpiki wakosolewa

PARIS, Ufaransa

MWANARIADHA mkongwe, Usian Bolt, amesaidia katika uzinduzi wa Mwenge wa Olimpiki kuelekea michezo hiyo itakayofanyika Paris 2024, lakini mashabiki walionekana kuchukizwa na muonekano wa mwenge huo.

Hiyo imetokana na muonekano huo kufananishwa na vitu vingi, lakini si kama Mwenge wa Olimpiki na Paralimpiki.

Bolt alionekana kuwa ni mgeni mwalikwa wakati wa utambulisho ukiendelea jijini hapa ikiwa imebaki mwaka mmoja kwenda kufanyika michezo hiyo nchini hapa.

Nyoya huyo anayeshikilia rekodi ya Dunia ya meta 100 na 200, alipewa Mwenge wa Olimpiki kutoka kwa Rais wa Ufaransa, Tony Estanguet mbele ya wanamichezo zaidi ya 1,000 pamoja na Rais wa IOC, Thomas Bach.

Lakini baadhi ya mashabiki walionekana kutofurahishwa na muundo wa mwenge huo ikifananishwa kama na chupa ya champagne na wengine kwenda mbali kama chupa ya ndani ya chai.

Mmoja wa mashabiki anaandika: “Kitu cha kwanza…tochi mbaya zaidi kuwahi kufanywa … inaonekana kama chupa ya champagne…nimekata tamaa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *