Arsenal yaipiga Barca 5-3

LOS ANGELES, Marekani

MCHEZAJI Leandro Trossard, amefunga mabao mawili wakati timu yake ya Arsenal ilipoitandika Barcelona 5-3 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanjani SoFi jijini hapa.

Mabao mawili ya Trossard ya kipindi cha pili yalikisaidia kikosi cha Kocha, Mikel Arteta kutoka nyuma na kuibuka na ushindi huo mbele ya mabingwa hao wa La Liga.

Wachezaji Bukayo Saka na Kai Havertz, ndio waliofunga mabao ya kusawazisha kwa Arsenal kipindi cha kwanza kabla ya mabao ya Trossard kuifanya Gunners kuwa mbele baada ya mapumziko.

Fabio Vieira alifunga bao la tano dakika za lala salama huku Ferran Torres akipoza machungu kwa kuifungia bao Barca.

Arsenal ambayo ni washindi wa pili wa Ligi Kuu England, itaanza msimu mpya kwa kuumana na Manchester City ambayo ilitwaa mataji matatu, kwa kucheza Ngao ya Jamii Agosti 6 uwanjani Wembley.

Ikiwa ni uwanja wa nyumbani wa timu za NFL, Los Angeles Rams na Los Angeles Chargers, nyota wa Barcelona, Robert Lewandowski, alifunga bao la kwanza baada ya dakika saba akiunganisha pasi ya Raphinha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *