‘Ndani ya Alcaraz kuna Nadal, Djokovic’

LONDON, England

MCHEZAJI mkongwe wa tenisi, Iva Majoli, amesema anaona vivuli vay wachezaji nyota, Rafael Nadal na Novak Djokovic ndani ya Carlos Alcaraz.

Mhispania Alcaraz, amejijengea heshima kubakia namba moja katika ubora wa viwango kwa kumtandika Djokovic katika mchezo uliokuwa wa seti tano wakati wa fainali ya Wimbledon mapema mwezi huu.

Hilo ni taji la pili kubwa kwa Alcaraz baada ya kutwaa la US Open mwaka jana, ikiwa ni taji lake la sita mwaka huu na 12 kwa ujumla katika mashindano yote.

Alcaraz amekuwa akifananishwa na mpinzani wake, Nadal, lakini Majoli ambaye alitwaa ubingwa wa French Open mwaka 1997, anaamini kuna visifa vya Djokovic ndani ya nyota huyo, 20.

Alipoulizwa yupi kati ya nyota watatu wa mchezo huo, Nadal, Djokovic na aliyestaafu Roger Federer anafanana kiuchezaji na Alcaraz, Majoli anaiambia Stats Perform: “Rafa ndiye alikuwa akimfuatilia wakati anakua na ni Mhispania, kwahiyo nitamuweka kwa ukaribu na Rafa, lakini nafikiri pia ana uchezaji fulani kutoka kwa Novak.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *