Madrid yaipiga Man Utd 2-0, Bellingham afunga

HOUSTON, Marekani

KIUNGO wa Real Madrid, Jude Bellingham, amefunga bao lake la kwanza akiwa na timu hiyo na kutajwa kuwa Mchezaji Bora wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Manchester United waliyoshinda 2-0 mjini hapa, Texas.

Kiungo huyo, 20 wa kimataifa wa England, hiyo ni mechi yake ya pili tangu asajiliwe kwa pauni milioni 88, alionesha kiwango bora na kufunga bao la kwanza dakika ya sita akimzidi ujanja kipa, Andre Onana.

Bao la pili la Madrid, lilifungwa na Joselu kwa tikitaka zikiwa zimebaki dakika mbilki mchezo kumalizika mbele ya mashabiki finish sealed the win two minutes from time 67,801 waliokuwepo uwanjani NRG.

“Tuna mengi tumeyadhamiria,” anasema Bellingham baada ya mchezo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *