Smith, Eubank Jr kurudiana Sept. 2

MANCHESTER, England

WAINGEREZA wapinzani, mabondia Liam Smith na Chris Eubank Jr, watapanda ulingoni kurudiana Septemba 2 katika pambano litakalofanyika ukumbini Manchester AO Arena.

Smith, 34, alimtandika Eubank Jr, 33, katika raundi ya nne mapema mwaka huu, na kufanya kuwa na gumzo kubwa kati yao.

Awali pambano hilo la marudiano lilipangwa kufanyika Julai Mosi, lakini lilihairishwa baada ya Smith kuumia mazoezini.

“Nipo fiti kwa sasa, nina majeraha, na ninachoangalia kwa sasa ni kwenda kummaliza Chris Eubank Jr,” amesema Smith.

Bondia huyo mzaliwa wa mji wa Liverpool, bingwa wa zamani wa WBO uzito wa kati, ameshinda mapambano 33 huku akipoteza matatu na sare moja.

Eubank Jr, ambaye ametaka kuwepo kwa pambano hilo la marudiano, ameshinda mapambano 32 na kupoteza matatu.

Kulikuwa na tetesi kwamba mazungumzo yake dhidi ya kuzichapa na Conor Benn yalifikia pazuri, lakini alisema pambano lake la marudiano dhidi ya Smith ni la kulipa kisasi.

Ameongeza: “Hakutakuwa na sababu, hakutahairishwa. Smith hawezi kukimbia milele.”

Promota wa pambano hilo, Ben Shalom, ameelezea pambano hilo ni mota kati ya mapambano gumzo katika mchezo wa ngumi Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *