Rais Samia, Mwinyi watajwa uzinduzi wa jezi Simba

Na Mwandishi Wetu, Mwanga

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, ni miongoni mwa viongozi ambao watakuwa na jezi maalum kutoka Klabu ya Simba watakapozindua jezi zao mpya za msimu wa 2023/24 Ijumaa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Mbali na viongozi hao, wengine ni Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

Akizungumza wilayani hapa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Iman Kajula, alisema watafanya uzinduzi siku hiyo saa 1 usiku na wamepandisha jezi tano zitakazokuwa na majina ya viongozi hao na ndizo zitakazotumika katika uzinduzi huo rasmi.

“Jezi zitakuwa na majina ya viongozi wa serikali mgongoni Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ally Mwinyi, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson na Rais wa Heshima Mohamed Dewji Mo,” amesema Kajula.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya, amekabidhi Bendera ya Taifa kwa mashujaa wa Simba ambao wataambatana na kibegi chenye jezi kwenda nacho hadi kileleni.

“Hichi kibegi kimetrendi sio tu Tanzania bali duniani kote, namimi nawahakikishia kitapewa ulinzi hadi kinafika kileleni na kurudi tena hapa,” amesema Mwaipaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *