LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema pauni milioni 100 za kumsajili Declan Rice zinaweza kuwa mnara wa taa na ni kiungo ambaye tulikuwa tunamuhitaji.
Rice, 24, alijiunga na timu hiyo akitokea West Ham kwa ada ambayo itaongezeka hadi kufikia pauni milioni 105.
Anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa ndani ya timu hiyo baada ya mshambuliaji Kai Havertz aliyetokea Chelsea kwa pauni milioni 65 na beki Jurrien Timber akitokea Ajax kwa pauni milioni 34.
Arsenal imeshika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City, licha ya kwamba ya kuongoza Ligi Kuu England kwa muda mrefu.
“Ninamuona kama mnara wa taa,” amesema Arteta akimzungumzia nyota huyo wa kimataifa wa England. “Yupo tayari kuwamulikia mwanga wengine, kuwasaidia wengine na kuifanya timu kuwa bora.
“Tumezungumza muda mfupi uliopita ni jinsi gani anaweza kucheza na kuwapongeza wachezaji na kuchukua njaa hiyo ya ushindi katika timu iliyotoka na kuwapa wachezaji ambao wanataka kujisukuma kwa kiwango tofauti
“Kwa uzoefu aliokuwa nao katika ligi atasaidi kuipeleka mbali zaidi timu hii. Ana sifa za kimwili ambazo tulikuwa tunakosa kwa muda
“Jinsi anavyozungumza na kujionyesha. Nia aliyonayo na mapenzi yake kwa mchezo ndiyo hasa tuliyohitaji.”
Rice alizuiliwa kufanya mazoezi ya baiskeli katika sehemu ya kwanza ya mazoezi huko Washington kabla ya mechi ya ufunguzi ya Arsenal ya msimu mpya leo dhidi ya timu ya akina Wayne Rooney ya MLS All-Stars.