VICTORIA, Australia
MICHEZO ya Jumuiya ya Madola, imefutwa na kuwaweka njia panda mashabiki wa michezo hiyo.
Michuano hiyo ijayo ya kipekee, ilitarajiwa kufanyika mjini hapa mwaka 2026.
Lakini Ofisa Habari wa michezo hiyo, Daniel Andrews, amethibitisha kufutwa kwa michezo hiyo kwa sababu ya kuongezeka kwa deni kwa jimbo la Australia na kusema “si uamuzi mgumu.”
Waratibu wa michezo hiyo wamepewa taarifa saa nane kabla ya taarifa hiyo kutolewa.
Mji wa Victoria ilipewa jukumu la kuandaa michezo hiyo mwaka jana.
Hilo ilitokana na kati ya mataifa 70 hakuna ambalo lilijitosa kuwania uenyeji wa michuano hiyo 2026.