LONDON, England
MCHEZAJI nyota katika tenisi, Novak Djokovic, amesema kupoteza fainali ya michuano ya Wimbledon mbele ya Carlos Alcaraz ni jambo gumu kulikubali lakini hana budi kusonga mbele.
Hisia alizokuwa akipata kwa kuwa mshindi wa pili huku akimwangilia mpinzani wake akiinua taji la ubingwa ambalo alilitwaa miaka minne iliyopita, kilimuumiza na kuanza kulia.
“Inaumiza,” amesema baada ya kushindwa kufikia rekodi ya kutwaa mara ya nane taji.
Djokovic, 36, amekuwa akisaka rekodi ya kumfikia mpinzani wake, Roger Federer kwa upande wa wachezaji wanaume pamoja na kumfikia Margaret Court kwa kufikisha Grand Slam 24 lakini alishindwa kufua dafu alipoumana na Alcaraz, 20.
Mhispania huyo ameshinda kwa seti 1-6 7-6 (8-6) 6-1 3-6 6-4 na kutwaa taji lake la pili kubwa, akimchapa Djokovic katika mchezo ambao mpinzani wake alitawala mchezo kwa muda mrefu uwanjani Centre Court.
Tangu mwaka 2013 Djokovic alipoteza katika mashindano ya ‘All England Club’ wakati Andy Murray alipomfunga na kutwaa ubingwa na nyota huyo alikuwepo uwanjani kumuangalia mserbia huyo.
“Ni ngumu kukubali wakati umekaribia,” amesema. “Nimepoteza mchezo kwa mchezaji bora na ninampongeza na ninasonga mbele.”