LONDON, England
BINGWA wa Dunia wa uzito wa juu, Tyson Fury, anatarajia kuzichapa na nyota wa mchezo wa MMA, Francis Ngannou katika pambano litakalofanyika Oktoba 28 nchini Saudi Arabia.
Bingwa huyo wa zamani wa UFC, Ngannou, 36, hana rekodi yoyote katika ngumi za kulipwa za kiweledi.
Timu ya Fury, amesema pambano hilo si la maonesho na litafanyika kwa kufuata kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa, kwa majaji watatu watakaofiuata mfumo wa alama 10.
Fury hatotetea mkanda wake wa WBC katika pambano hilo la mjini Riyadh.
“Huyu mtu atakuwa anarusha ngumi kali zaidi ulimwenguni, lakini ngoja tuone nitakavyopambana naye ulingoni,” amesema Fury.
Kwa upande wa Ngannou, alisema ni ndoto iliyokuwa kweli kupanda ulingoni na Fury.