Na Sarah Moses, Dodoma.
MKUTANO Mkuu Maalum wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) unatarajiwa kufanyika kesho jijini Dodoma kwaajili yakupiga kura kwa wagombea Ubunge Vitimaalum upande
makundi maalum ambapo Wajumbe zaidi ya 1000 watashiriki mkutano huo.
Akizungumza leo Julai 1,2025 Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema kuwa maandalizi yote yamkutano yameshakamilika huku akiwaalika Wajumbe wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuhudhuria mkutano huo.
Amesema kuwa kila baada ya miaka 5 UWT hufanya uchaguzi wa viongozi wa serikali nakuongeza kuwa mkutano huo utahusisha upigajikura kwa makundi maalum 4.
“Makundi hayo ni pamoja na Asasi za Kiraia, Wasomi wa Vyuo Vikuu, Wafanyakazi pamoja na Watu wenye ulemavu” amesema.
Amesisitiza kuwa Waliochaguliwa siyo kwamba wamepita mojakwamoja bali kinyanganyiro kinaendelea hivyo wanapaswa kufanya kampeni ili kuhakikisha chama kinapata kura za kutosha zitakazowezesha nafasi za viti maalum kuwa nyingi.
Amesema kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu imeteua wagombea 8 kwenye kila kundi huku akiwaaasa Wajumbe kupiga kura kwa watu wanaowapenda wao nasiyo aliyewapa kitu.
“Wakachague viongozi kwa haki na siyo waliotoa rushwa kwani chama chetu kumeshaelekeza nakupiga vi ya rushwa.
” Tunaelewa wagombea wamekuja na wapambe wao hivyo basi Wajumbe wanatakiwa kuwa makini”amesema Chatanda.
Katika hatua nyingine Chatanda amewasisitiza wagombea watakao chaguliwa kuwania nafasi hizo wasibweteke kwani bado safari ni ndefu yakuweza kuchaguliwa .
“Ushindi wa kura siyo uteuzi bado kuna Vikuu vingine ambavyo vitaendelea kuchuja hivyo waendelee kuomba kura .
Mwisho.