Zifahamu dhana 7 potofu kuhusu ukomo wa hedhi

Na Mashirika ya Habari

SIKU ya Ukomo wa Hedhi Duniani huadhimishwa kila mwaka Oktoba 18 kwa lengo la kuongeza uelewa na kuondoa unyanyapaa unaokumba mamilioni ya wanawake wanaopitia hali hiyo ya kibiolojia.

Ulimwenguni, idadi ya wanawake waliofikia ukomo wa hedhi inaongezeka kwani wanawake wanaishi muda mrefu zaidi.

Mnamo 2021, wanawake wenye umri wa miaka 50 na zaidi walikuwa 26% ya wanawake na wasichana wote duniani. Hii ilikuwa kutoka 22% kutoka miaka 10 kabla kulingana na data ya Umoja wa Mataifa.

Licha ya ukoma hedhi kuwa hatua ya kawaida katika maisha ya mwanamke mara nyingi huwa haieleweki.

Masuala kuhusu ukoma hedhi zinaendelea kujadiliwa kote duniani. Hapa kuna dhana saba za kupotosha kuhusu ukweli unaowazunguka hali hii:

Ukomo wa hedhi ni sawa kwa wanawake wote. Mabadiliko ya homoni hutatofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine kulingana na mambo ya kijamii na kitamaduni, kibaolojia na maisha. Mabadiliko haya huenda yakatofautiana kulingana na mtindo wa maisha wa kila mwanamke.

Ukomo wa hedhi hutokea katika miaka ya hamsini

Ingawa wastani wa umri wa ukoma hedhi ni miaka 51, inaweza kuanza katika umri wa miaka 40 na 60 – hutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine na makabila tofauti.

Ni lazima utaongeza uzani ukifikia ukomo wa hedhi

Uwezo wa mwili kufanya kazi hupungua kadri umri wa mtu unavyoongezeka bila kujali athari za ukoma kwa hedhi. Madaktari wanapendekeza kufanya mazoezi mara kwa mara na kula chakula bora ili kusaidia kudhibiti uzzani wa mwili kwa afya njema.

Jasho kupita kiasi ni jambo la kawaida na dalili pekee ya ukomo wa hedhi

Kutokwa na jasho kupita kiasi ni jambo la kawaida wakati wa ukomo wa hedhi lakini sio wanawake wote wanapitia hali hiyo. Hujitokeza zaidi katika miaka miwili ya kwanza ya ukoma hedhi na kwa kawaida hupotea baada ya miaka saba katika 60% ya wanawake waliofikia hali hiyo.

Ukomo wa hedhi huathiri hamu ya ngono

Ukavu katika sehemu ya uke, kutokuwa na hamu ya kufanya tendo ngona na sonona henda ikachangia kupungua kwa ashiki. Hata hivyo, kwa usaidizi wa mhudumu wa afya na wenzi wenye walio na uelewa wanawake wanaweza kuendelea na maisha ya kawaida na kufurahia tendo la ndoa.

Ukomo wa hedhi husababisha unyogovu, wasiwasi na mabadiliko ya hisia

Kukoma hedhi hakusababishi unyogovu bali matatizo ya usingizi na kuhisi joto kupita kiasi ambayo ni hali ya kawaida miongoni mwa wanawake waliokoma hedhi na inaweza kuchangia kuwa na hasira na hali ya kubadilika-badilika.

Tiba ya homoni ina hatari nyingi za kiafya

Ingawa kutumia tiba ya homoni kunaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya matiti kunaweza pia kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa. Tafiti zinaonyesha kuwa manufaa yanaweza kuzidi hatari kwa wanawake wenye afya na walio na umri wa chini ya miaka 60 amao wanakabiliwa na tatizo la kutokwa na jasho kupita kiasi wakifikia ukomo wa hedhi.

Ukomo wa hedhi ni nini?

Kukoma hedhi kunatokea wakati kuna mabadiliko katika homoni za ngono kadri wanawake wanaopata hedhi wanavyozeeka. Ovari huacha kutoa mayai kila mwezi na viwango vya estrojeni hupungua. Kukoma hedhi kwa kawaida hutokea kati ya umri wa miaka 45 na 55 – lakini kwa wengine kunaweza kutokea mapema zaidi.

Kwa kawaida ishara iliyowekwa ni ya kutopata hedhi kwa miezi 12 mfululizo – ambayo haiwezi kuhusishwa na sababu ya kibayolojia au ya kisaikolojia. Ni ishara ya mwisho wa miaka ya rutuba na uzazi ya mwanamke.

Lakini hedhi haitokei mara moja. Mchakato huo kwa kawaida huwa wa taratibu huku kipindi cha mpito kikichukua wastani wa miaka saba, hata hivyo kwa baadhi ya wanawake inaweza kuwa hadi miaka 14.

Kukoma hedhi hufanyika katika hatua tatu za kimsingi:

Ya kwanza ni kabla ya kukoma hedhi, ambayo huathiri wanawake wengi walio na umri wa miaka 30 na 40 mapema. Katika kipindi hiki, wanawake bado wanapata hedhi mara kwa mara, lakini viwango vya estrojeni na progesterone vinaweza kuanza kubadilika.

Pili, kipindi cha kukoma hedhi ambacho kinaonyesha mwisho wa uzazi katika maisha ya mwanamke, viwango vya estrojeni hushuka kwa kiasi kikubwa. Katika hatua hii, hedhi inakuwa isiyo ya kawaida, na wanawake wanaweza kukosa hedhi, mzunguko mfupi wa hedhi au mizunguko mirefu ya hedhi. Wanawake wanaweza pia kupata mafua kali, wasiwasi na kukosa usingizi.

Na hatimaye, baada ya kumaliza hedhi, ambayo inahusu muda baada ya mwanamke kukosa hedhi kwa miezi 12 mfululizo. Katika hatua hii, dalili nyingi zinazopatikana wakati wa kukoma kwa hedhi hupungua polepole.

Kuna dalili tofauti hadi 48 za ukomo wa hedhi, kulingani na Shirika la Afya Duniani, WHO. Dalili za kawaida ni pamoja na: kutokwa na jasho sana hata kama ni wakati wa baridi na kuhisi joto nyakati za usiku, mabadiliko ya kawaida na mtiririko wa mzunguko wa hedhi na kusababisha mwisho wa hedhi, ukavu wa uke, maumivu wakati wa kujamiiana, gumu wa kulala au kukosa usingizi, kubadilika kwa hisia, unyogofu, na/au wasiwasi, kudhofika kwa viungo, kupungua kwa ukubwa wa mifupa ambayo huchangia viwango vya juu vya osteoporosis na na kuvunjika.

Dalili hizi zote zinatokea wakati ambao homoni za mwanamke za ‘estrogen’ ikiwa chini sana.

Ni muhimu kutambua kwamba sio wanawake wote wanapata dalili hizi – lakini wengi wana, karibu 75%.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *