Kasi ya Rais Samia yamvutia mbunge CUF kuhamia CCM

Na Mwandishi Wetu, Handeni

KASI ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kufungua demokrasia nchini inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan imemvutia Mbunge wa zamani wa Viti Maalum wa Chama cha Wananchi (CUF), Sonia Magogo na wengine 25, kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Magogo, ambaye alikuwa Mbunge wa CUF wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Tanga kati ya mwaka 2015-2020 na mgombea ubunge katika Jimbo la Handeni Mjini 2020, alijiunga na CCM Jumamosi, Februari 10, 2024 wakati wa mkutano wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdallah, uliofanyika kwenye Kata ya Chanika.

Mkutano huo ni muendelezo wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya Rais Samia ambapo alisema ni muhimu watendaji wa chama na serikali kumsaidia Rais katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Sonia alisema yeye na vijana wengine 25 wameamua kuhama CUF kwa sababu wananchi wa Handeni walimuonyesha ushirikiano.

Mbunge huyo aligombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa 2020 kupitia Chama Cha Wananchi, (CUF) na kupata kura 6,713, huku Reuben Kwagilwa wa CCM alishinda kwa kura 15,241.

“Kazi kubwa anayoifanya mheshimiwa rais wetu wa Jamhuri, mama aliyejaa busara, mama anayejali, mama mwenye kuipenda nchi yake, imenisukuma leo kuja kuungana nanyi ili tuongeze nguvu kuhakikisha Tanzania inasonga,” alisema Magogo.

Akaongeza: “Lakini kwa namna ya kipekee nimpongeze Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga kwa namna anavyojitahidi kukijenga chama. Hili nalo limenisukuma kwa kujua kwamba CCM ni sehemu salama. Nina imani pia na viongozi wote wa Mkoa wa Tanga wa Chama cha Mapinduzi kwa kuwa najua siyo kazi ya mwenyekiti peke yake mpaka leo hii CCM inaendelea kushamiri katika mkoa huu.

“Nimeona hakuna sababu ya kuendelea kuvutana, tunahitaji maendeleo, tunahitaji kupiga hatua katika Mkoa wa Tanga, hivyo hatuna muda wa kuendelea kulumbana. Kwa pamoja tunaweza.

“Lakini maamuzi haya sijayafanya peke yangu. Nina wenzangu ambao nimeandamana nao. Pamoja nami nimeandamana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CUF Mkoa wa Tanga na Katibu wake.”

Baada ya kuwapokea wanachama hao, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah ameonya wanachama wa chama hicho kutowanyanyasa wenzao wageni, kwani ni haki ya kila mtu kuchagua chama anachotaka.

Mbunge wa Handeni Mjini Reuben Kwagilwa akimkaribisha aliyekuwa mgombea mwezie kupitia CUF Sonia katika uchaguzi wa 2020 amesema kwa kurudi kwake CCM, wana uhakika wa kuwa hakuna upinzani kwenye

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *