Tumieni Takwimu za Sensa 2022 – Makinda

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMISHNA wa Sensa nchini, Anne Makinda, amesema kwa sasa ni ruksa kwa mdau yeyote kutumia taarifa ya matokeo ya sensa ya mwaka 2022.

Makinda ambaye ni Spika wa Bunge mstaafu, aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Arusha na Manyara kwenye mafunzo ya uwasilishaji, usambazaji na uhamasishaji matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi.

Alisema tanzania imekuwa bora zaidi katika takwimu za sense, haijapata kutokea katika Bara la Afrika hivyo wadau wanaweza kuzitumia kwa ustawi wa Taifa, maendeleo ya wananchi.

Alieleza kuwa, upatikanaji taarifa sahihi na kutumika kikamilifu inaisaidia serikali na wadau wengine kuwatumikia wananchi.

“Sensa hii ni makini na haijawahi kutokea barani Afrika isipokuwa hapa Tanzania, bila ninyi waandishi wa habari tusingeweza kufanikisha,” alisema.

Aliongeza kuwa, matokeo ya sense mwaka 2022 baada ya kutangazwa, ulitoka mwongozo wa kukutanisha makundi mbalimbali, kuyapa taarifa hizo wakiwemo wanahabari.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya usimamizi Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Amina Msengwa, alisema senda hiyo haikuwa rahisi kuwafikia Watanzania milioni 61 kwa wakati bali mafanikio yalitokana na ushirikiano wa waandishi wa habari katika kuuhabarisha umma.

Mkuu wa Mkoa huo, John Mongola, alisema jamii imepata elimu ya umuhimu wa sensa ambapo katika dunia ya sasa taarifa za sensea ni jambo muhimu sana.

“Tumepata elimu ya kutosha kujua nini maana ya sensa, katika dunia ya sasa ya sayansi ya teknolojia, bila kuwa na takwimu sahihi hakuna matumizi sahihi,” alieleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *