Na Mwandishi Wetu
WAKATI joto la Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Marekani uliopangwa kufanyika Novemba 5, mwaka huu likipanda, Kampuni nyota ya Michezo ya Kubashiri nchini, LEONBET, imetangaza kuwapa fedha watakaobashiri kiusahihi matokeo ya wagombea, Donald Trump na Kamala Harris.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa LEONBET Tanzania, Tumaini Maligana, wameamua kupanua wigo wa kubashiri kwa wafuatiliaji wa siasa ili na wao waweze kufaidika kupitia ubashiri wao.
Maligana amesema hiyo ni nafasi yao ya kipekee ya kutumia maarifa yako kushinda fedha kupitia uchaguzi wa Marekani ambao unatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwa wagombea hao wawili.
“Cha kuvutia zaidi, sasa unaweza kubeti matokeo haya kupitia LEONBET, kampuni mpya ya kubashiri nchini Tanzania iliyokuja na nguvu kubwa, odds za kibabe na malipo fasta,” amesema Maligana.
Katika hatua nyingine, Maligana akizungumzia ukuaji wa kasi kwa kampuni yao hapa nchini, amesema kwa zaidi ya miaka 15 katika sekta ya kubashiri, LEONBET imefanikiwa kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wateja wake ulimwenguni kote.
“Sasa, kampuni hii yenye uzoefu mkubwa imekuja Tanzania na inaleta mabadiliko makubwa kwenye soko la kubeti mtandaoni.
“Kwa watumiaji wa Tanzania, LEONBET inaleta mambo mengi ya kuvutia kama Odds kubwa, beti zako zinaweza kukupatia ushindi mkubwa zaidi na pili malipo ya haraka ambayo uwawezesha washindi kupata malipo papo hapo,” amesema.
Pia amesema kampuni yao imepanua wigo wa kubashiri ambayo inawapa fursa wapenda michezo, siasa au burudani na vile vile kuwapa nafasi ya kubeti bure hadi kufikia sh. 8, 000 kwa wateja wapya.
“Unapojisajili leo, unabeti bure hadi sh. 8, 000 kwenye mwezi wako wa kwanza. Hii ni nafasi yako ya kuanza bila ya kuwekeza fedha zako mwenyewe na kuongeza nafasi yako ya kushinda.” amesisitiza.