Pluijm kuitumia AS Vita kusuka kikosi

KOCHA Mkuu wa timu ya Singida Fountain Gate, Hans Pluijm, amesema atautumia mchezo wao wa kesho dhidi ya AS Vita ya DR Congo ili kujua ubora na upungufu wa kikosi chake kabla ya kuanza msimu mpya.

Singida FG itaumana na AS Vita katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa utakaopigwa Uwanja wa Liti mkoani hapa ikiwa ni kilele cha Tamasha la Singida Big Stars.

Akizungumza kuelekea maandalizi ya tamasha hilo, Pluijm anasema kikosi chake kipo vizuri kwa mchezo huo na watauutumia kujua mambo mbalimbali ya kiufundi kuelekea msimu mpya.

“Hautakuwa mchezo rahisi tunajiandaa kupambana na nina kikosi kipya, hivyo Jumatano tutakuwa na mchezo mzuri dhidi ya AS Vita ili kufahamu ubora na upungufu yetu,” anasema Pluijm.

Viingilio katika tamasha hilo ni sh. 3,000 kwa mzunguko na VIP ni sh. 5,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *