Skudu aahidi mataji Yanga

Na Zahoro Mlanzi

KAZI imeanza! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Winga mpya wa timu ya Yanga, Mahlatse Skudu Makudubela, kuahidi kuwapa raha wanayohitaji wanachama na mashabiki wa timu hiyo.

Nyota huyo, 33, mwenye udambwi udambwi mwingi katika kuchezea mpira, alitambulishwa usiku wa manane kuamkia jana huku akipewa jezi namba 6 ambayo ilikuwa ikiimbwa na kunadiwa kwa muda mrefu.

Awali jezi hiyo ilikuwa ikivaliwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye amejiunga na Azam FC baada ya kushindwa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Skudu ambaye mkataba wake haujawekwa wazi, amesajiliwa akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambayo ilitolewa na Yanga katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kwenda kushuka daraja katika ligi yao.

Akizungumza kwa ufupi baada ya kutambulishwa rasmi, Skudu amesema:” Wana-Yanga, wananchi…Skudu nipo hapa, umekiona ulichokipenda, nipo hapa kukupa ulichopenda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *